Migiro ataka vijana wasiendelee kuachwa kando

28 Februari 2012

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha –Rose Migiro amesema kuwa serikali pamoja na watunga sera wanakazi kubwa ya kufanya ili kutambua nguvu za uzalishaji walizonazo vijana. 

Pia amehimiza haja ya kuwepo kwa mageuzi ili kutatua tatizo la kimfumo linaloendelea kuwaacha vijana wengi nje ya ajira.

 Katika hotuba yake wakati akifungua kongamano la kimataifa lililoandaliwa na baraza la uchumi na masuala ya kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, Migiro amesema kuwa kuendelea kukosekana kwa ajira kwa makundi mengi ya vijana, ni kichocheo kinachopalilia mikwamo ya kisiasa na ile ya kijamii.

 Amesema matukio mengi yaliyoshuhudiwa yakijiri katika maeneo mbalimbali,kama huko Brooklyn, Cairo, Barcelona, Tunis na Tripoli ni matokeo yanayoelezea matatizo yanayowaandama vijana.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter