Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu lafanya majadiliano

Baraza la Haki za Binadamu lafanya majadiliano

Baraza la haki za binadamu limeendesha majadiliano kwa ajili ya kumulika hali ya haki za binadamu huku likiweka zingatio la kuwepo kwa mashirikiano ya kimataifa.

 Katika ujumbe wake kupitia video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi wanachama wa Umoja huo zinawajibika kuheshimu na kuzingatia masuala ya haki za binadamu.

Amezitolea mwito nchi wanachama kuendeleza mazingira yatayotoa mwanga kwa wananchi kufurahia mienendo inayoheshimu na kukuza haku za binadamu.

Kwa upande wake Kamishna wa haki za binadamu Bi Navi Pillay amesema kuwa kuwepo kwa ongezeko la mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoweka msukumo wa masuala ya haki za binadamu kumeleta msukumo mpya ambao unahimiza namna masuala ya haki za binadamu yanavyopaswa kutekelezwa katika ngazi zote.