Mshindi wa tuzo ya Oscar ataka kutengeneza filamu kuhusu UM

27 Februari 2012

Mshindi wa tuzo ya filamu yaani Oscar Terry George amesema moja ya mimitadi yake ijayo itakuwa kutengeneza filamu kuhusu mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa Sergio Viera de Mello ambaye aliuawa katika shambulio la bomu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Iraq mwaka 2003.

Bwana George ameshinda tuzo ya filamu bora fupi iitwayo “The Shore” inayohusu vijana wawili waliokuwa katika sehemu mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa machafuko Ireland ya Kaskazini.

George ambaye pia alitengeneza sinema ya Hotel Rwanda, amekuwa akichukua hadithi ya kitabu cha Samanta Powers kiitwacho ‘Chasing the Flame: Sergio Viera de Mello and the fight to save the Work” akitaka kukitengeneza kuwa filamu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter