Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawahamisha kwa muda wafanyakazi wake baada ya shambulio kaskazini mwa Afghanistan

UM wawahamisha kwa muda wafanyakazi wake baada ya shambulio kaskazini mwa Afghanistan

Umoja wa Mataifa unawahamisha kwa muda wafanyakazi wake wa kimataifa kutoka katika ofisi yake ya mpango wa kulinda amani UNAMA iliyoko jimbo la Kuunduz Kaskazini mwa nchi hiyo kufuatia kuongezeka kwa ghasia.

Ofisi hizo zilishambuliwa mwishoni mwa juma na waandamanaji wenye hasira kutokana na wanajeshi wa Marekani kuchoma kitabu kitakatifu cha Koran wiki iliyopita.

Hakuna mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyeadhirika japo kulikuwa na vifo upande wa majeshi ya usalama ya Afghanistan na baadhi ya waandamanaji.

Kwa mujibu wa UNAMA  kuhama huko ni kwa muda na mpango huo utaendelea kutoa msaada unaohitajika kwa jimbo la Kunduuz. Marekani imeomba radhi kwa kuchomwa kwa Koran na kusema ilikuwa ni ajali ya bahati mbaya.