Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamhuri ya Afrika ya kati yazindua kampeni ya kutokomeza polio

Jamhuri ya Afrika ya kati yazindua kampeni ya kutokomeza polio

Kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya polio imezinduliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa juma ikiwa na lengo la kufikiwa watoto wote nchini humo ikiwa ni pamoja na wale ambao ni vigumu kuwafikia wanaoishi kwenye maeneo ya vita na ambako vita ndio vimemalizika tuu na hivyo huduma za afya ni haba.

Kampeni hii ambayo imeazimia kutokomeza kabisa polio ni hatua ya haraka iliyochukuliwa kudhibiti visa vipya vinne vya polio vilivyobainika kuingia nchini humo mwaka 2011 ambavyo ni visa vipya vya kwanza baada ya miaka miwili. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)