Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na IFAH kukabiliana na biashara haramu ya dawa za mifugo

FAO na IFAH kukabiliana na biashara haramu ya dawa za mifugo

 

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula la kilimo FAO na shirikisho la kimataifa la afya ya mifugo IFAH wanafanya kazi pamoja ili kuanzisha viwango vya kwanza vya sekta ya madawa kwa ajili ya dawa zinazotumika kutibu ugonjwa unaoathiri mifugo Afrika ujulikanao kama Nagana au malale.

Kwa mujibu wa Juan Lubroth mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya mifugo matumizi ya madawa yasiyo na viwango kutibu maradhi ya malale sio tu kwamba yanawaacha mifugo bila ulinzi dhidi ya maradhi hayo bali pia yanazidisha usugu dhidi ya dawa kutokana na kutopewa dawa zinazostahili.

Ugonjwa wa malale ambao unaambukizwa kwa kuumwa na mbung’o, unauwa mifugo ambao wakulima wadogowadogo ndio tegemeo lao barani Afrika, kwa maisha yao ya kila siku. Pia maradhi hayo duniani kote yanakadiriwa kusababisha hasara ya dola hadi bilioni 4.5 kila mwaka.