Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Angola imekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika vita dhidi ya polio: Ban

Angola imekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika vita dhidi ya polio: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza Angola kwa juhudi zake za kutokomeza ugonjwa wa polio.

Katika risala yake kwenye kituo cha chanjo ya polio mjini Luanda Jumatatu Ban amesema matokeo ya juhudi hizo ni kuwa huru bila polio mwaka 2001, lakini amelaumu kwamba katika kipindi cha miaka minne baadaye virusi vya polio vimerejea.

Amesema ndio maana ni muhimu sana kuendelea na kampeni kama iliyozinduliwa leo Jumatatu,  na ni muhimu kufuatilia hali inavyokwenda ili kuweza kukabiliana na mlipuko wa maradhi hayo haraka.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)