Baraza la haki za binadamu lafanya mjadala wa dharura kuhusu Syria

27 Februari 2012

Baraza la haki za binadamu litafanya mjadala wa dharura kuhusu hali ya Syria licha ya Iran kupinga kufanyika kwa mjadala huo. Mjadala utafanyika Jumanne kwa ombi maalumu la Qatar amesema Rais wa baraza la haki za binadamu Laura Dupuy Lasserre. Rais huyo pia amesema amepokea pingamizi rasmi la mjadala huo kutoka kwa Iran ambayo sio mwanachama kati ya wanachama 47 wa baraza la haki za binadamu bali ni mwangalizi. Akizungumza katika mwanzo wa kikao cha 19 cha baraza hilo kamishina mku wa haki za binadamu Navi Pillay na wajumbe wengine wengi wa Umoja wa Mataifa wamekaribisha hatua ya kufanyika kwa mjadala huo kuhusu Syria. Rais wa baraza la haki za binadamu Laura Dupuy Lasserre amesema ana matumaini kwamba baraza litakuwa na maamuzi ya pamoja kulaani ghasia zinazoendelea Syria na kudai fursa za kuweza kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yaliyoathirika.

(SAUTI YA LAURA DUPUY LASSERRE)

Pillay ameongeza kuwa licha ya hatua zilizopigwa kuna mengi ambayo baraza linaweza kuyafanya katika kutimiza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba watu wote katika mataifa yote wanatekelezewa haki zao za binadamu. Amesema baraza linapaswa kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu lakini kuna hali ambazo zinahitaji kushughulikiwa haraka zaidi.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter