Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM akaribisha kurejea kwa wafanyakazi Kordofan Kusini:

Mratibu wa UM akaribisha kurejea kwa wafanyakazi Kordofan Kusini:

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Mark Cutts amekaribisha kurejea leo kwa wafanyakazi wa kimataifa ambao ni wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kordofan Kusini.

Hatua hii imefuatia uamuzi uliofanywa awali na serikali ya Sudan wa kuidhinisha kurejea kwa wafanyakazi hao, na wafanyakazi wawili wa kwanza wamewasili leo kwenye mji mkuu wa jimbo hilo Kadugli.

Jana serikali ya Sudan iliwasilisha matokeo ya tathimini ya hali ya kibinadamu Kordofan Kusini , tathimini iliyoendeshwa na tume ya serikali ya misaada ya kibinadamu na ilimulika maeneo ambayo yanadhibitiwa na serikali. Bwana Cutts amesema anatambua juhdi zilizofanywa na serikali pamoja na mashirika ya kibinadamu ya kitaifa na kimataifa katika kushghulikia mahitaji ya kibinadamu kwenye jimbo hilo. Ametoa wito wa tathiomini kufanyia pia katika maeneo yote yaliyoathirika na vita yanayodhibitiwa na serikali na yanayodhibitiwa na kundi la SPLM-North.

Amesisitiza kwamba kinachotakiwa hivi sasa ni kukomesha mapigano ili watu wasiendelee kutawanyika bali kurejea makwao. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na Umoja wa nchi za Kiarabu wametoa pendekezo la pamoja ili kuwezesha watu kfikiwa katika maeneo yaliyoathirika na vita Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile.