Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kutupia macho watoto walioko mijini: UNICEF

Ni wakati wa kutupia macho watoto walioko mijini: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema zaidi ya watu bilioni 7 duniani hivi sasa wanaishi mijini, na h ii inamaanisha nini kwa watoto? .

Kwa mujibu wa shirika hilo ripoti yake ya mwaka 2012 imetenga maalumu kwa ajili hiyo, kuangalia hali ya watoto duniani husani wale wanaokulia mijini. Miji inajulikana kwa kukuza uchumi lakini ripoti hiyo inasema sio watoto wote wanaofaidika na upanuzi wa miji, kwani katika ukuaji huo wa miji bila kuwa na mtazamo Imara kuhusu haki za watoto maana yake watoto wengi wanasahaulika.

Ripoti hiyo itaweka bayana kwamba ukiukaji mkubwa wa haki za watoto za kuishi, huduma za afya, elimu na ulinzi umeenea maeneo ya mijini, ingawa miji hiyohiyo ndio hutoa huduma muhimu bora zaidi kuliko vijijini. Watoto wengi ambao haki zao hazitimizwi ni pamoja na wale wanaoishi mitaa ya mabanda, watoto wa mitaani, walio katika sekta zisizo rasmi na watoto wahamiaji.

Kutokuwepo usawa ni hali inayojitokeza duniani kote ingawa mifumo inatofautiana. Ripoti hiyo itatoa wito wa kuwepo kwa juhudi za pamoja ili kuzipa kipaumbele haki za watoto katika wakati wa kufanya maamuzi mijini ili kupunguza pengo na kujenga mustakhbali bora wa maisha ya mijini.

Ripoti hiyo ya hali ya watoto duniani mwaka 2012 itatolewa tarehe 28 Februari na inajikita katika watoto wanaoishi maeneo ya mijini.