Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yanayoendelea yatakiwa kuwa na mazingira bora ya kibiashara

Mataifa yanayoendelea yatakiwa kuwa na mazingira bora ya kibiashara

Mataifa yanayoendelea yametakiwa kufanya jitihada za kuhakikisha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kibiashara ikiwa yatahitaji kuwa na fedha za kugharamia miundo msingi yao.

Hii ndiyo ilikuwa ajenda kwenye mkutano wa mwaka huu wa watunza sera kuhusu ushirikiano kati ya washika dau wa kibinafsi na wale wa umma PPP. Kwa sasa ushirikiano wa PPP unakabiliwa na changamoto za hali mbaya ya kiuchumi huku mashirika mengi ya kifedha yakikawia kutoa mikopo.George Njogopa na taarifa kamili.