Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wengi wana nia ya kuhamia nchi za kigeni

Watu wengi wana nia ya kuhamia nchi za kigeni

Imebainika kuwa watu wazima milioni 630 duniani wanaweza kuhamia nchi zingine kabisa. Hii ni kulingana na matokeo ya utafiti wa taasisi ya utafiti duniani Gallup. Ripoti hiyo inatoa picha nzuri kwa mara ya kwanza kuhusu maisha ya watu walio na nia ya kuhama kabisa au kufanya kazi kwa muda, wanajiandaa kuondoka na waliorejea nyumbani.

 Ripoti hiyo inayochambua matokeo ya mahojiano yaliyofanyiwa watu 750,000 duniani kote tangu mwaka 2005 imeelezea kwa undani wahamiaji ni nani , wanatoka wapi, jinsi wanavyoishi, wanaweza kuenda wapi na hii ina maana gani kwa serikali , mashirika ya umma na washika dau.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa nchi 18 zinawavutia zaidi ya asilimia 70 ya wahamiaji duniani huku Marekani ikiongoza kama nchi inayowavutia wahamiaji wengi zaidi ikifuatiwa na Canada, Uingereza , Ufaransa na Hispania. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.