Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aihakikishia Zambia usaidizi wa Umoja wa Mataifa

Ban aihakikishia Zambia usaidizi wa Umoja wa Mataifa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaisaidia nchi ya Zambia katika jitihada zake za kuboresha uchumi za kuhakikisha kuwepo kwa ajira na kupunguza umaskini.

Kwenye ujumbe wake kwa bunge la Zambia Ban amesema kwamba kitu muhimu kwa taifa la Zambia ni watu wake akiongeza kuwa Zambia itagundua umuhimu wakati wanawake na vijana pia watagundua umuhimu wao.

Ban alilitaka taifa hilo kufanya jitihada za kuwashirikisha vijana na wanawake kwenye maendeleo ili waweze kufaidika na kuboreka kwa uchumi kwa maisha yao ya siku baadaye. Ban amesema kuwa vijana wanahitaji elimu bora na mafunzo ya kuwawezesha kupata ajira za kisasa.