Ukosefu wa usawa kwenye maeneo ya kazi waongezeka barani Ulaya

24 Februari 2012

Shirika la ajira duniani ILO limesema kuwa kutokuwepo usawa kwenye maeneo ya kazi kumeongezeka barani Ulaya hasa kutokana na hali mbaya ya uchumi na hali hiyo inatarajiwa kuendelea wakati nchi nyingi zinapoendelea kufanya mabadiliko kwenye masuala ya ajira.

Kulingana na utafiti wa ILO ni kwamba hali kwenye maeneo ya kazi, mishahara na usawa wa kijinsia mingoni mwa masula mengine yamekuwa yakidorora kote barani Ulaya tangu kuanza kwa hali mbaya ya uchumi.

Utafiti huo unaonyesha kwamba wafanyikazi walio kwenye kandarasi za muda waliathirika zaidi huku mfano ukitolewa nchini Hispania ambapo asilimia 90 ya kupotea kwa ajira iliwaathiri wafanyikazi wanaofanya kazi kwa kandarasi za muda. Hans von Rohland ni kutoka ILO

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter