Watu 130,000 wakimbia makwao kufuatia mapigano yanayoendelea nchini Mali

24 Februari 2012

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa zaidi ya raia 130,000 wa Mali wamelazimika kuhama makwao kufuatia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Tuareg kwenye eneo la kaskazini mwa nchi. Watu 63,000 wamehama ndani mwa nchini huku waliosalia wakikimbilia nchi majirani zikiwemo Niger, Burkina Faso, Mauritania na Algeria.

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Matifa OCHA linasema kuwa kwa sasa lengo kuu ni kuwapelekea misaada waliohama makwao kwa sababu huenda hali ikawa mbaya zaidi kutokana na ukame uliopo kwenye eneo la Sahel. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linahitaji kwa dharura dola milioni 35 ili kukabiliana na hali hiyo. Adrian Edwards ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter