Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna ongezeko la ukosefu wa usawa sehemu za kazi: ILO

Kuna ongezeko la ukosefu wa usawa sehemu za kazi: ILO

Utafiti mpya uliotolewa na shirika la kazi ulimwenguni ILO, unaonyesha ongezeko kubwa la ukosefu wa usawa sehemu za kazi.

Utafiti huo unasema hali ya kukosekana kwa usawa kwenye sehemu za kazi barani Ulaya ni kubwa na kuonya kwamba mwenendo huo unatazamiwa kuendelea kushuhudiwa kwa kipindi kIrefu.

Kwa mujibu wa utafiti huo mabadiliko hayo yamechangiwa pakubwa na mkwamo wa kiuchumi uliojitokeza miaka ya hivi karibuni.

Wakati huu nchi nyingi barani Ulaya zinajaribu kusaka njia za kukabiliana na matokeo ya kuyumba kwa uchumi ikiwemo pia kufanyia mageuzi sheria za kazi, kitendo ambacho kinaelezwa kuzidisha ukosefu wa usawa kazini.