Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakusanya nguvu ya pamoja kukabili janga la njaa

Wakusanya nguvu ya pamoja kukabili janga la njaa

Huku kukisubiriwa kwa hamu kubwa kuzinduliwa rasmi kwa filamu inayozungumzia njaa, waandaaji wa filamu hiyo wameanza kukutana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP kwa ajili ya kuhamasisha ulimwengu juu ya kitisho cha njaa.

Tayari wamezindua wavuti ambao ndani yake inapatikana picha za video zinazoelezea mchezo kuhusiana na janga la njaa.

Zingatio kubwa linalowekwa na pande zote, ni kuoimba jumuiya mbalimbali duniana kuunga mkono jitihada za kukabiliana na tatizo la njaa.

Tatizo la njaa ambalo hata hivyo linaweza kutafutiwa ufumbuzi, linaelezwa kuwakabili mabilioni ya watu duniani wote. Kwa sasa takwimu zinaonyesha kuwa kila penye watu 7 basi mmoja wao anakabiliwa na tatizo la njaa.