Kofi Annan kwenda kusuluhisha Syria

24 Februari 2012

Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu umemteua Bwana Kofi Annan kuwa mjumbe maalumu atayeshughulia mzozo wa Syria. Wakati pande hizo mbili zikimtangaza Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa kushughulikia mzozo huo, taarifa kutoka nchini humo zinaeleza hali inavyozidi kuwa mbaya.

Mamia ya watu wameendelea kupoteza maisha kutokana na operesheni kali inayoendeshwa na vikosi vya serikali dhidi ya wananchi. Katika kusaka suluhu ya mzozo huo, Koff Annan anatazamiwa kusaidia na mjumbe mwingine atakayechaguliwa hivi karibuni kutoka nchi mojawapo ya Jumuiya ya kirabu.

Viongozi hao wanatazamia kuanzisha duru la majadiliano kwa shabaha ya kukomesha machafuko hayo na hatimaye kulirejesha taifa hilo kwenye utengamao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter