Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi, Tanzania na UNHCR kuwarejesha nyumbani wakimbizi walioko Mtabila

Burundi, Tanzania na UNHCR kuwarejesha nyumbani wakimbizi walioko Mtabila

Serikali ya Burundi, Tanzania na na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameazimia kufunga kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Mutabila iliyoko nchini Tanzania ifikapo mwezi wa Disemba mwaka huu.

Halmashauri hiyo ya pande tatu imetangaza hatua hiyo katika kikao cha 16 kilichofanyika alhamisi hii mjini Bujumbura Burundi na kutaja kwamba hamna tena sababu za msingi za wakimbizi hao kusalia nchini Tanzania.

Shughuli ya kuwarejesha kwa hiari wakimbizi takribani elfu 37 itaaanza rasmi mwezi wa April. Tanzania imetoa tahadhari kwa wakimbizi watakaokaidi amri hiyo kwamba watachukuliwa kama wahamiaji haramu.

Mbali na wakimbizi 162,000 waliopewa uraia wa Tanzania, hadi sasa Tanzania inawapa hifadhi wakimbizi 67,000 kutoka Burundi. Na tangu shughuli hiyo kuanzishwa mwaka wa 2002, tayari wakimbizi 500,000 wamerudi makwao.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA ameandalia makala hii.

(PKG NA RAMADHAN KIBUGA)