Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aongeza muda wa kimamlaka kwa mahakama ya kimataifa juu ya mauwaji ya Hariri Lebanon

Ban aongeza muda wa kimamlaka kwa mahakama ya kimataifa juu ya mauwaji ya Hariri Lebanon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameidhinisha kwa miaka mingine mitatu mahakama ya kimataifa inayofuatilia mauwaji ya aliyekuwa kiongozi wa Lebanon Rafik Hariri, mahakama ambayo ilitazamia kumaliza muhala wake wa kwanza Machi mwaka huu.

Mahakama hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inaendesha mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa mauwaji ya waziri mkuu huyo wa zamani,mauwaji yaliyofanyika mnamo mwaka 2005.

Bwana Hariri na wenzake wengine 22 waliuwawa siku ya February 14, kufuatia shambulizi la bomu lililolenga msafara wake mjini Beirut.

Tayari watuhumiwa kadhaa ikiwemo Salim Jamil Ayyash, Mustafa Amine Badreddine, Hussein Hassan Oneissi na Assad Hassan Sabra, wote wakiwa raia wa Lebanoni wamefikishwa kwenye hahakama hiyo wakituhumiwa kuhusika juu ya mauwaji hayo.