Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahalifu wa ubakaji katika maeneo ya vita watajwa na kuaibishwa:

Wahalifu wa ubakaji katika maeneo ya vita watajwa na kuaibishwa:

Kukomesha matumizi ya ubakaji na mifumo mingine ya ukatili wa kimapenzi kama kutumika kama silaha za vita bado ni moja ya changamoto kubwa katika kulinda haki za binadamu amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya vita.

Bi Margot Wallstrom amesema njia moja ya kupambana na ukwepaji wa sheria ni kuwataja na kuwaaibisha wahusika wa uhalifu huo. Amesema kuwa kwa mara ya kwanza orodha hiyo ya majina imejumuishwa katika ripoti ya kila mwaka ya Katibu Mkuuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa leo.

Ameongeza kuwa nia ni kuweka mazingira ambayo makundi ya wapiganaji wenye silaha wataona ukatili wa kimapenzi ni kama chanzo kitakachowakaribisha uchunguzi wa kina wa kitaifa na kimataifa.