Wakulima wadogowadogo kufaidika na ushirikiano baina ya IFAD na wakfu wa Gates

23 Februari 2012

Taarifa iliyotolewa na mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD inasema ushirikiano imara baina ya wakfu wa Bill na Melinda Gates na mfuko huo unamaanisha kuboresha msaada kwa wakulima wadogowadogo duniani.

Taarifa ya muafaka imetiwa saini Alhamisi wakati wa kikao cha baraza la IFAD kwenye makao makuu mjini Roma, kati ya mwenyekiti mwenza wa wakfu wa Bill na Melinda Gates ambaye ni Bill Gates na Rais wa IFAD Kanayo F. Nwanze.

Makubaliano yao yatajikita katika ushirikiano na kuinua shughuli za pamoja katika kuwasaidia wakulima wadogowadogo kwenye nchi zinazoendelea. Wakulima wanakabiliwa na changamoto mbili kubwa katika miongo minne ijayo. Ni lazima wazalishe asilimia 60 zaidi ya chakula kulisha ongezeko kubwa la watu duniani, huku wakikabiliwa na hatari za uharibifu wa mazingira, upungufu wa rasilimali na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter