Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri kwenye mkutano wa UM wakubaliana kuchukua hatua za kuleta maendeleo

Mawaziri kwenye mkutano wa UM wakubaliana kuchukua hatua za kuleta maendeleo

Mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani wameafikiana kuhakikisha kuwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo utakaoandaliwa nchini Brazil baadaye mwaka huu utafanikiwa kupata suluhu za changamoto za kimazingira duniani.

 Mawaziri hao wanasema kwamba mkutano wa Rio +20 ambao utafanyika mjini Rio de Janeiro utakuwa fursa nzuri ya kujadili changamoto za kiuchumi ,kijamii na kimazingira kwa minajili ya maendeleo.

Kupitia taarifa wakati wa kukamilika kwa mkutano wa siku tatu wa baraza la shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP uliofanyika kwenye makao makuu ya UNEP mjini Nairobi Kenya ulisema kuwa changamoto za kimazingira zilizoangaziwa kwenye mkutano za mwaka 1992 zimeanza kuonekana.