Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Togo inafaa kuongeza kiwango cha fedha zinazotumika katika vita dhidi ya Ukimwi:UNAIDS

Serikali ya Togo inafaa kuongeza kiwango cha fedha zinazotumika katika vita dhidi ya Ukimwi:UNAIDS

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi Michel Sidibe amesema serikali ya Togo inapaswa kuongeza kiwango cha fedha zinazotumika katika vita dhidi ya ukimwi nchini humo. Sidibe ameyasema hayo alipozuru nchi hiyo na kubaini kwamba Togo inategemea sana fedha kutoka nje ili kufadhili zaidi ya asilimia 80 ya mapambano yake dhidi ya ukimwi.

Sidibe ameitaka serikali kuwekeza kiasi kikubwa kutokana na vyanzo vya fedha vya ndani. Akizungumza na waziri mkuu wa Togo Houngbo mjini Lome amesema itakuwa ni vigumu kumpa mgonjwa dawa za kupunguza makali ya ukimwi kwa miaka 30 wakati taifa likitegemea fedha kutoka nje. Amesema itawezekana tu endapo pamoja na kutegemea msaada wa nje kuwa na suluhisho la Afrika yenyewe.