Wafungwa 44 wauawa kwenye gereza moja nchini Mexico

Wafungwa 44 wauawa kwenye gereza moja nchini Mexico

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeutaka utawala nchini Mexico kufanya uchunguzi ulio huru kufuatia mauaji ya wafungwa 44 kwenye gereza moja kaskazini mwa nchi mauaji yaliyotekelezwa na wanachama wa kundi moja lililojihami.

Wafungwa wengine 26 wengi wanaokabiliwa na hukumu ya kifo walifanikiwa kutoroka gerezani katika jimbo la Nuevo Leon siku ya Jumapili. Msemaji kwenye ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani anasema kuwa uchunguuzi ni lazima ufanyike kuhusu mauji hayo na pia kuhusu kukimbia kwa wafungwa kutoka gerezani.