Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa ya amani imewekwa bayana Somalia: Ban

Fursa ya amani imewekwa bayana Somalia: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameuuambia mkutano wa kimataifa kuhusu Somalia unaofanyika mjini London kwamba Umoja wa mataifa umefungua mlango kwa ajili ya kupatikana kwa amani na utulivu nchini Somalia.

Katika mkutano huo wa Alhamisi unaojumuisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali ya mpito ya Somalia, wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, makundi ya jumuiya za kijamii , Umoja wa Mataifa na wadau wengi wanaopigania amani ya Somalia Ban amesema ingawa fursa yenyewe ni ndogo lakini inatoa nafasi ambayo ni ya muhimu sana na ni gharama kubwa kuikosa, fursa ya kuwasaidia watu wa Somalia na kumaliza vitisho na hali ya kutokuwa na usalama iliyomea mizizi kwa zaidi ya miongo miwili.

Ameongeza kuwa hii ni fursa ya kutambua mtazamo wa maendeleo na hatma ya amani ya Somalia na ametoa wito wa kuimarisha hatua za usalama, kuboresha mchakato wa kisiasa na kuongeza msaada wa ujenzi mpya na maendeleo ya taifa hilo.