Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maharamia watengeza dola milioni 170 kama fidia kutokana na utekaji nyara wa meli mwaka jana

Maharamia watengeza dola milioni 170 kama fidia kutokana na utekaji nyara wa meli mwaka jana

Maharamia wametengeneza mamilioni ya dola mwaka jana kutokana na utekaji nyara wa meli na wafanyakazi wake.

Yury Fedetov ameliarifu Baraza la Usalama juu ya tatizo la uharamia katika pwani ya Somalia, ambalo ni tatizo linaloendelea.

Ameonya kwamba biashara hii ya uharamia inafanya bei kuongeza katika pembe ya Afrika.

Bwana Fedotov amesema fedha hizi kutoka kwa uharamia zinatumika katika shughuli zingine za uhalifu kama madawa ya kulevya, silaha na magendo, na usafirishaji haramu wa binadamu.