Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wadogo wanaweza kuulisha ulimwengu IFAD

Wakulima wadogo wanaweza kuulisha ulimwengu IFAD

Wakulima wadogo wametakiwa kuchukua wajibu mkubwa katika kuulisha ulimwengu miaka inayokuja. Hili ni kwa mujibu wa wataalamu wanaohudhuria mkutano ulioandaliwa na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD.

Huku idadi ya watu duniani ikitarajiwa kugonga watu bilioni 9 ifikapo mwaka 2050 IFAD inasema kwamba wakulima wadogo wanaweza kuchangia kuwepo usalama wa chakula duniani. IFAD inasema kwamba kuwepo kwa masoko na hali nzuri ya hewa wakulima hawa wadogo wanaweza kuchangia mabadiliko kwenye jamii zao. Dola bilioni 1.5 zilichangishwa ili kufadhili miradi ya kilimo kwenye nchi zinazoendelea