Ziara kuhusu masuala ya nyuklia iliyofanywa Iran yakosa kuzaa matunda

22 Februari 2012

 

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na nishati ya nyuklia limeelezea kuhuzunishwa kwake na kutokuwepo mafanikio wakati wa ziara ya siku mbili iliyofanywa nchini Iran ili na lengo la kubainisha shughuli za kinyuklia za taifa hilo.

Kundi la wataalamu kutoka kwa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA walifanya mazungumzo na maafisa kutoka Iran kati ya tarehe 20 na 21 mwezi huu mazungumzo yaliyojiri baada ya yale ya awali yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita. Ziara ya juma hili ilikuwa na lengo la kusuluhisha utata uliopo kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran mpango ambao Iran inautaja kuwa wa amani huku mataifa mengine yakiuona kama ulio na lengo la kuunda zana za kinyuklia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter