Japan yafadhili huduma za afya kwenye kanda ya Gaza

22 Februari 2012

Serikali ya Japan imetoa msaada wa dola milioni 10 kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA kwa vituo kumi vya afya kwenye ukanda wa Gaza mwaka huu. Makubalino hayo yalitiwa sahihi kwenye mji wa Amman kati ya kamishina mkuuu wa UNRWA Filipo Grandi na balozi wa Japan nchini Jordan Junichi Kosuge.Monica Morara na taarifa Kamili.

Kamishina Filipo aliwaambia waandishi wa habari kuwa moyo wa kusaidia kutoka kwa taifa la Japan ni mkubwa mno hasa ikikumbukwa kuwa taifa la Japan lilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi. Japan inachukua nafasi ya 11 kama mmoja wa wafadhili wakubwa wa shirika la UNRWA huku pia ikifadhili miradi ya dharura.

Mwaka uliopita Japan ilichangia Dola milioni 15 kwa shirika la UNRWA na imetoa ufadahili mkubwa kwenye ujenzi wa kambi ya Nahr el- Bared kaskazini mwa Lebanon iliyoharibiwa mwaka 2007.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter