Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko yanahitajika kwenye usimamizi wa masuala ya mazingira duniani

Mabadiliko yanahitajika kwenye usimamizi wa masuala ya mazingira duniani

Kunahitajika mabadiliko makubwa ya jinsi ulimwengu unavyosimamiwa iwapo changamoto za dunia zingehitaji kutatuliwa kwa watu bilioni saba. Hii ni kutokana na mapendekezo kutokana na utafiti uliondeshwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kupitia kwa wanasayansi 400 na wataalamu wengine kutoka kote duniani.

Mkurugenzi mkuu wa UNEP Achim Steiner anasema kuwa mpango huu umechangia kuwepo kwa maono makubwa kuhusu changamoto zinazoikumba dunia. Waiganjo Njoroge ni afisa wa  shirika la UNEP mjini Nairobi na anafafanua zaidi.

(SAUTI YA WAIGANJO NJOROGE)