Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza wanajeshi wa kikosi cha AMISOM nchini Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza wanajeshi wa kikosi cha AMISOM nchini Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kuongezwa kwa wanajeshi wa kulinda amani kwenye kikosi cha Muungano wa Afrika cha kulinda amani nchini Somalia AMISOM kutoka wanajeshi 12,000 hadi wanajeshi 17,000. Kwenye azimio lililopitishwa leo Jumatano baraza hilo pia liliamua kuongeza usaidizi unaotolewa na Umoja wa Mataifa kwa kikosi hicho.

Kikosi cha AMISOM ambacho asilimia kubwa ya wanajeshi wake wanatoka nchini Burundi na Uganda kinaisaidia serikali ya mpito nchini Somalia kuchukua udhibiti na kupigana na wanamgambo wa Al-Shabaab. Balozi Mark Lyall Grant kutoka Uingereza ambaye alipendekeza azimio hilo anasema kuwa uamuzi huo ni muhimu katika kuleta utulivu nchini Somalia.