Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil ndiyo itakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani

Brazil ndiyo itakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limetangaza kuwa taifa la Brazil ambalo ni moja ya mataifa yaliyo na uchumi unaokua kwa haraka zaidi duniani itakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani mwaka 2012 ambayo itaadhimishwa tarehe 5 mwezi Juni.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Uchumi usioathiri mazingira: Inakuhusu wewe ?' ina lengo la kumkaribisha kila mmoja na kuhakikisha kuwa maendeleo kupitia masuala haya yanafikia uchumi usioathiri mazingira na yanaweza kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yanayohitajika kwenye ulimwengu wa sasa wenye watu bilioni saba. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(SAUTI YA GRACE KANEIYA)