Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka wahusika wa uchomaji Koran Afghanistan washughulikiwe

UM wataka wahusika wa uchomaji Koran Afghanistan washughulikiwe

Umoja wa Mataifa umesema kuwa unamatumaini umoja wa kujihami NATO uanoongoza vikosi vya kijeshi nchini Afghanistan utachukua hatua muhimu ili kuwawajibisha wale wote waliohusika na uchomaji moto wa vitabu vya Korani Kabul ambako kumesababisha maandamano makubwa na watu kadhaa kupoteza maisha.

Sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo imetangaza kuanzisha uchunguzi wa haraka juu ya namna tukio hilo la uchomaji moto lilivyotendeka.

Tangu kuarifiwa kwa tukio hilo, mamia ya waandamanaji wamekusanyika kwenye kambi iliyoko vikosi vya Marekani Bagram nje kidogo ya mji wa Kabul ambako ndiko tendo la kuchomwa moto nakala za Koran lilifanyika.

Wakati hali hiyo ikiendelea , Afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amekutana na maafisa wa serikali na kufanya majadiliano nao.