Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa UNAMID warejea nyumbani

Wanajeshi wa UNAMID warejea nyumbani

Baada ya mazunguzmo marefu sasa kundi la wanajeshi 55 wa kupiga doria wa kikosi cha pamoja cha Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kwenye jimbo la Darfur UNAMID ambacho kilikuwa kimezuiwa na wanamgambo waliokuwa wamejihami kaskazini magharibi kwa muda wa siku mbili sasa kimeelekea kwenye makao yake kwenye eneo la Umm Baru.

Mkuu wa kikosi hicho Bwana Ihrahim Gambari amempongeza kamanda wa kikosi hicho Luteni Patrick Nyamvumba pamoja na Brigadia Mansamusa Monde na wanajeshi waliojipata kwenye hali hiyo. Bwana Gambari anaongoza kikosi cha wanajeshi 26,000 wa UNAMID walio na jukumu la kulinda raia kwenye jimbo la Darfur.