Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa amani wa UM awataka wasanii wachanga kuchora picha za ulimwengu usio na zana za kinyuklia

Mjumbe wa amani wa UM awataka wasanii wachanga kuchora picha za ulimwengu usio na zana za kinyuklia

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa Michael Douglas ametoa wito kwa watoto kutoka kote duniani kuwasilisha fikra zao kwa njia ya sanaa kuhusu ni vipi ulimwengu  usio na zana za kinyuklia utakavyokuwa. Bwana Douglas ambaye amehudumu kama mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1998 ametoa ujumbe kupitia kwa ukanda wa video ambapo amewataka wasanii wachanga kuanzia umri wa miaka 5 hadi 17 kutumia vipawa vyao na kuchora michoro ya kuashiria ulimwengu usio na silaha za kinyuklia.

 Kwenye ujumbe uliotangazwa kwenye vituo mbali mbali duniani Douglas alisema kuwa sanaa huongea hadi ndani mwa akili na roho za binadamu.