Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Onyo la kutokea mafuriko latolewa Ulaya

Onyo la kutokea mafuriko latolewa Ulaya

Onyo la kutokea kwa mafuriko limetolewa kwenye maeneo ya mashariki na kati kati mwa Ulaya wakati barafu iliyoanguka wakati wa kipindi cha msimu wa baridi inapoanza kuyeyuka. Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na mjanga inasema kuwa nchi zinazopakana na mto Danube ziko kwenye hatari kubwa ya kufurika.

Ofisi hiyo inasema kuwa inatarajia viwango vikubwa vya maji kutoka kwa theluji inayoyeyuka na huenda ikawa mtihani mkubwa kwa nchi za Ulaya tangu kutokea kwa mwafuriko miaka 10 iliyopita. Denis Mcclean ni msemaji wa shirika la kupambana majanga la Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA DENIS MCCLEAN)