Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM aitaka Israel kumwachilia huru mfungwa wa Kipalestina aliye kwenye mgomo wa kula

Mjumbe wa UM aitaka Israel kumwachilia huru mfungwa wa Kipalestina aliye kwenye mgomo wa kula

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayejishughulisha na haki za binadamu katika mamlaka ya Palestina amerejelea tena mwito wake kuitaka Israel kumwachilia huru mfungwa wa Kipalestina ambaye yupo kwenye mgomo wa kutokula chakula.

Mjumbe huyo Richard Falk amesema Israel inapaswa kumwachilia huru mfungwa huyo Khader Adnan ambaye anaripotiwa kudhoofika kwa hali ya afya yake kutokana na mgomo huo wa kutokula.

Sasa anaingia siku ya 66 ya kutokula chakula kama njia ya kupinga vitendo vya kionevu na matunzo mabaya anayoyapata kutoka kwa mamlaka ya Israel.

Hali ya afya yake inaarifiwa kudhoofika na kuna wasiwasi pengine akapoteza maisha.