Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa DRC

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa DRC

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa kwenye eneo la Bas-Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tangu mwanzo wa mwaka huu ambapo kumeripotiwa visa 125 na vifo vya watu watano huku ugonjwa huo ukisambaa kwenye mikoa tisa kati ya mikoa 11.

Kwa muda wa miezi sita zaidi ya dola milioni 13 zimetengwa kwa vita dhidi ya kipindupindu zikiwemo dola milioni tisa zilizotengwa mwezi Januari mwaka huu. Ukosefu wa maji umesalia kuwa changamoto kubwa linalochangia kurejea mara kwa mara kwa ugonjwa huo wakati taifa hilo linapojaribu kujitoa kwenye janga lililosababisha vifo vya watu 644 na kuwaathiri wengine 26,000 tangu Januari mwaka 2011.