UM wazitaka pande zinazopigana Sudan Kusini kusaka njia mwafaka ya kutanzua mizozo

21 Februari 2012

Maafisa wa Umoja wa Mataifa walioko huko Sudan Kusini wamezionya pande zinazopigana kutafuta njia mwafaka ya kupatikana kwa suluhu na hatimaye kutuma ujumbe utaotafsiri maridhiano yanayoweza kupatikana bila kuendelea kuathiri mamia ya watu.

Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa pande zinazozozana zina kila sababu ya kumaliza mkwamo huo kwa njia ya maelewano na wala sio kuendeleza vita na machafuko ambayo kimsingi yanamaliza maisha ya raia.

Wamesema kuwa kwa kufanya hivyo pande hizo zitafaulu kutuma ujumbe kwa makabila mengine nchini humo kwamba kuna njia sahihi ya kufikia suluhu na siyo kuendeleza mapigano ya kikoo.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo Hilde F. Johnson,ametembelea maeneo yaliyokumbwa na machafuko na kufungua kongamano la siku tatu lenye shabaha ya kujadilia hali ya amani

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter