Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan yafadhili miradi ya maji nchini Somalia

Japan yafadhili miradi ya maji nchini Somalia

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanzisha uchunguzi wa miezi mitatu kuhusu usambazaji wa maji na usafi kwa wakimbizi wa ndani wanaoishi kwenye vitongoji vya mji mkuu wa Somalia Mogadishu. Mpango huo umefadhiliwa na taifa moja kutoka Japan ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwepo kwa huduma bora za maji zitakazowafaidi maelfu ya watu kweye mji wa Mogadishu baada ya taifa hilo kukumbwa na ukame mbaya zaidi kuwai kulikumba kwa muda wa miaka 60 iliyopita.

Mradi huo pia utahakikisha kuwepo kwa maji kwenye kambi za wakimbizi ukitumia teknolojia kutoka Japan kupitia kwa kampuni ijulikanayo kama Nippon Poly- Glu.