Rais wa Baraza Kuu la UM akutana na mwanadiplomasia wa Misri

21 Februari 2012

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Misri kujadilia hali ya kisiasa nchini humo wakati ambapo vugu vugu la mageuzi katika mataifa ya kiarabu likitoa taswira mpya ya mageuzi.

Wakikutana katika mji mkuu Cairo, viongozi hao rais Nassir Abdulaziz Al-Nasser na mwenyeji wake wamejadilia hatua muhimu zilizopigwa na nchi hiyo tangu kumalizika kwa vugu vugu la mapinduzi lililomwondosha rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak.

Rais huyo ameipongeza Misri kwa juhudi zake za kufanikisha kipindi cha mpito kwa kuendesha uchaguzi wa bunge ambayo inatoa matumaini mapya kwa wananchi wa taifa hilo.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohamed Kamel Amr amekaribisha ziara za kiongozi huyo na kuarifu namna wananchi wa taifa hilo walivyo tayari kusonga mbele

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter