Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yaomba misaada ya kusaidia mataifa kwenye eneo la Sahel

Mashirika ya UM yaomba misaada ya kusaidia mataifa kwenye eneo la Sahel

Maisha ya karibu watu milioni moja kwenye eneo la Sahel barani Afrika yako hatarini kutokana na kuwepo utapiamlo na magonjwa yanayoambukiza.Mashirika ya Umoja wa Matifa katika eneo hilo yanasema kuwa ukosefu wa ufadhili wa kutosha umekuwa kizuizi katika utoaji misaada kwa watoto huku hali hiyo ikiendelea kuwa mbaya kila siku.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa kutokea kwa mikurupuko ya magonjwa ya surua na kipindupindi nchini Niger na Chad huenda yakaifanya hali kuwa mbaya zaidi ikiwa magonjwa hayo hayatadhibitiwa.

Nalo shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa limefanikiwa kuchangisha dola milioni 11 kati ya dola milioni 120 zinazohitajika ili kukabiliana na hali kwenye eno la Sahel. Marixie Mercado ni kutoka shirika la UNICEF mjini Geneva