Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walitaka bara la Afrika kuwekeza zaidi kwenye nishati safi

UM walitaka bara la Afrika kuwekeza zaidi kwenye nishati safi

Sera za serikali zinazochangia uwekezaji wa kibinafsi kwenye kawi ni muhimu katika kupunguza umaskini kwenye bara la Afrika na kulielekeza kwenye maendeleo. Hii ni kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo. Wataalamu wanasema kwamba ikiwa hatua mwafaka hazitachukuliwa nusu ya watu wote kwenye bara la Afrika bado watakuwa bila umeme ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo kutoka kwa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mjini Nairobi nchini Kenya inaonyesha kuwa vizuizi vilivyo sasa vya kupata kawi barani Afrika kama vile gharama ya juu ya kupata kawi vinaweza kusuluhishwa. Msemaji wa UNEP mjini Nairobi Nick Nuttall alizungumza na Monica Morara wa Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu uzinduzi wa ripoti hii.

(SAUTI YA NICK NUTTALL)