Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wazungumzia kufungwa kwa watetesi wa haki za binadamu nchini Syria

Wataalamu wa UM wazungumzia kufungwa kwa watetesi wa haki za binadamu nchini Syria

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameshutumu kukamatwa kwa takriban watu 16 wakiwemo watetesi maarufu wa haki za binadamu nchini Syria wakisema kuwa huenda watu hao wakateswa. Wanasema kuwa huenda watu hao wamekamatwa kutokana na sababu zinazohusiana na uhuru wa kujieleza na shughuli za kutetea haki za binadamu. Wataalamu hao wanaongeza kuwa utawala nchini Syria ni lazima ukomeshe dhuluma dhidi ya watetesi wa haki za binadamu na kuwaachilia wote waliokamatwa bila ya sababu. George Njogopa anaripoti.