Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia yataka uwekezaji zaidi katika kupunguza majanga

Mataifa ya kusini mashariki mwa Asia yataka uwekezaji zaidi katika kupunguza majanga

Maafisa wa ngazi za juu serikalini kutoka eneo la kusini mashariki mwa Asia wametaka kuwe na uwekezaji katika maandalizi dhidhi ya majanga kwa minajili ya kulinda uchumi na masuala mengine ya kijamii. Wawakilishi kutoka mataifa yakiwemo Brunei, Darusssalam, Cambodia, Jamhuri ya Lao, Myanmar, Ufilipino, Timor-Leste, Thailand na Viet Nam walikutana kwenye warsha iliyoandalia na tume ya masuala ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa.

Pia maafisa hao walijadili waliojifunza kutokana na mafuriko ya mwaka 2011 na jinsi ya kuyandaa mataifa yao kwa majanga siku za usoni. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)