Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa shirika la misaada ya dharura asikitikia hali mbaya Sudan

Mkuu wa shirika la misaada ya dharura asikitikia hali mbaya Sudan

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa shirika la misaada ya kibinadamu ameelezea kile alichokiita kupindukia kwa hali ya ubinadamu katika jimbo la Kordofan lililoko Sudan Kusini ambalo linaandamwa na machafuko.

Bi Valerie Amos amesema hali jumla kwenye jimbo hilo na lile la Blue Nile ni ya kukatisha tama katika wakati ambapo hali ya utengamao wa kibinadamu ikizidi kuanguka.

Mamia ya watu wanaendelea kupoteza maisha kutokana na mapigano yanayozuka mara kwa mara na hivyo kuvuruga kabisa hali ya ustawi wa kibinadamu

Bi Amos, ambaye pi ni mratibu wa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Sudan pamoja na kundi la waasi la SPLM kuheshimu na kutekeleza makubaliano waliyofikiwa chini ya kivuli cha Umoja wa Mataifa kuhurusu wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kiutu kuwasili kwenye eneo hilo .