Kuadhimisha Siku ya Urithi duniani

20 Februari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametaka kuwepo maendeleo ya kiuchumi ili kuhakikisha kuwepo kwa urithi duniani. Kwenye ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya urithi duniani inayoadhimishwa tarehe ishirini ya kila mwezi Februari kila mwaka Ban amesema kuwa mabadiliko makubwa yameshuhudiwa duniani hasa misururu ya maandamanio iliyoshudiwa kwenye nchi kadhaa.

Ban amesema kuwa mkutano wa Umoja wa Mataifa  utakaoandaliwa mjiji Rio De Janeriro mwezi Juni utazipa serikali na watunza sera fursa ya kufirikiria mikakati mipya ya maendeleo yenye mafanikio siku za baadaye. Nalo shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linalosherekea siku hii linasema kuwa elimu ni muhimu kwa maendeleo ya urithi duniani.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud