Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walibya wanaelekea kuwa na demokrasia :BAN

Walibya wanaelekea kuwa na demokrasia :BAN

Ban Ki-moonKatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki –moon hii leo ameadhimisha mwaka mmoja tangu kuanza mapinduzi nchini Libya ambapo amewataka wananchi wa Libya kushirikiana ili kuwa na demokrasia iliyopatikana kwa njia ya haki.

Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa usaidizi wake nchini Libya wakati wa kipindi cha mabadiliko hasa kwenye uchaguzi wa bunge na pia kwenye jitihada za kutafuta katiba.

 Ban amewataka walibya kusimama kwa pamoja na kuwa na uwiano akisema mabadiliko hayastahili kuwa sababu ya ukiukaji wa haki za binadamu bali ni ya kuhakikisha kuwa wanamwake , vijana na mashirika ya kijamii wanashiriki vilivyo kwenye maendeleo