Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wataka kuwepo mkataba dhabiti kuhusu biashara ya silaha

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wataka kuwepo mkataba dhabiti kuhusu biashara ya silaha

Wakuu wa mashirika kadha ya kibinadamu , maendeleo na haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa wanaotoa huduma kubwa wamependekeza masuala kadha yatakayojumuishwa kwenye mkataba wa biashara ya silaha hasa kufuatia athari za kimaendeleo za biashara hii isiyo na usimamizi mwema.Wakuu hao wamesema kuwa sheria za sasa za kudhibiti biashara ya silaha hazina uwezo. Wameongeza kuwa athari za kibinadamu zinazotokana na suala hilo ni kubwa na matumuzi mabaya ya silaha ni ya juu.